AHADI ZAKE
Nafsi yangu usichoke
Roho yangu msifu Bwana
Aliahidi atatenda
Tumainiye Bwana
Ahadi zake ni za milele
Akiahidi atatenda
Roho yangu nafsi yangu
Tumainiye Bwana
Chorus
Kama mvua ishukavyo
Toka mbinguni kwenye ardhi
Na neno lake kwa kinywa chake
Halitarudi bure
Litatimiza mapenzi Yake
Litatenda aivyosema
Roho yangu nafsi yangu
Tumainiye Bwana
Mawazo Yake sio yetu
Njia zake si kama zetu
Mbingu zilivyo juu ya nchi
Mawazo Yake ni makuu
Ataagiza fadhili zake
Wimbo Wake kwangu usiku
Sifadhaike usiiname
Tumainiye Bwana
Back to Hymn List