SI NJIA RAHISI

Si njia rahisi, yakwenda mbinguni,
Njiani ina miba mingi,
Si njia rahisi tunaye Mwokozi
Kuwa naye ni furaha kuu.

CHORUS
La, La si njia rahisi (x2)
Kutembea na Yesu huongoza safari,
Mazito huyarahizisha

Si njia rahisi, majaribu na shida
Ajali nyingi twazikuta,
Mbali Yesu yuko, kutukinga na yote
Hurahizisha njia zetu.

Roho mara huchoka, safari ni ndefu
Nami hufa moyo kwa mengi
Siku njema yaja, kwetu huko
mbinguni
Na kupumzika milele.
Back to Hymn List