NIWONAPO MTI BORA

Niwonapo Mti bora
Kristo aliponifia
Mwangu pato ni hasara
Kiburi nakichukia.

Na nisijivune, Bwana,
Ila kwa mauti yako;
Upuzi sitaki tena,
Zi chini ya damu yako.

Tangu kichwa hata nyayo
Zamwagwa pendo na hamu,
Ndako pweke hamu hiyo,
Pendo zako zimetimu.

Vitu vyote vya dunia
Si sadaka ya kutosha,
Pendo zako zaniwia
Nafasi, mali, ya maisha.
Back to Hymn List