IMANI NI KITU CHA MAANA

Imani ni kitu cha maana
Mkristo apaswa kuwa nacho,
Dunia pasipo na imani,
Hatuwezi kumpendeza Mungu.

CHORUS
Kwa imani twaokoka
Kwa imani tunaponywa,
Kwa imani tunajazwa,
Kwa imani twafika mbinguni.

lbrahim kwa imani,
Akamtoa mwanawe
Isaka Awe kafara ya kuteketea,
Akaitwa Rafiki wa Mungu.

Yoshua naye kwa imani,
Akazunguka Yeriko mara saba
Kuta za mji zikaanguka
Akateka mji kwa imani.
Back to Hymn List